Sure Boy amerejea kikosini

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Apr 2026
Sure Boy amerejea kikosini

Baada ya kukosekana tangu mwanzo wa msimu huu, kiungo mkongwe wa Yanga Salum Abubakar 'Sure Boy' jana alirejea kwa mara ya kwanza akipata dakika chache kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons.

Mchezo huo uliopigwa uwanja wa KMC Complex, uliishuhudia Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0 na kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi.

Furaha ya mashabiki wa Yanga haikuwa ushindi tu, urejeo wa Sure Boy uliibua shangwe kubwa wakati alipotambulishwa uwanjani.

Duke Abuya alimkabidhi kitambaa cha unahodha katika kutambua heshima yake ndani ya klabu ya Yanga.

Baada ya dakika 90 za mchezo huo, mashabiki wakaendeleza utamaduni wao kwa 'kumtuza' Sure Boy pamoja na Abuya ambaye nae aling'ara katika mchezo huo.

Kwa muda mrefu mashabiki wa Yanga walitamani kumuona Sure Boy dimbani, hatimaye benchi la ufundi limesikia kilio chao.

Bila shaka wachezaji wengine kama Farid Mussa na Kibwana Shomari nao watapata nafasi katika mechi zijazo.

Baada ya kikao cha tathmini ya mechi za duru ya kwanza, uongozi wa Yanga uliagiza benchi la ufundi kuhakikisha linawatumia wachezaji wote kwa kuzingata mahitaji ya mechi ili kupunguza athari za uchovu na majeruhi kwa wachezaji wanaotumika zaidi.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
2h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
7h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
7h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’