Matchday; Yanga vs Prisons, NBC PL, April 04

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Apr 2026
Matchday; Yanga vs Prisons, NBC PL, April 04

Baada ya mapumziko ya takribani wiki mbili, mabingwa watetezi wa ligi kuu ya NBC, Yanga leo wanarejea dimbani wakiwakaribisha Tanzania Prisons katika mchezo utakaopigwa uwanja wa KMC Complex.

Ni zaidi ya dakika 270 zimepita tangu Yanga iliposhinda mchezo wa ligi kuu hivyo ni wazi leo watashuka dimba la KMC Complex wakiwa na morali kubwa ya kusaka ushindi.

Wanakutana na Tanzania Prisons ambayo tangu ujio wa kocha Chadrack Nsajigwa imeimarika zaidi mara ya mwisho timu hizo zikikutana kwenye mchezo uliopigwa uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma na Yanga ikachomoza na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Depu dakika ya 80.

Tanzania Prisons wako katika nafasi mbaya kwenye msimamo wa ligi hivyo kwao kila mechi ni kama fainali wakati Wananchi wanafahamu vyema kama watakosa alama tatu leo, basi wanaiweka rehani nafasi yao pale juu ya msimamo.

Habari njema kwa Yanga ni kurejea kwa baadhi ya wachezaji waliokuwa majeruhi hasa nyota wa kikosi cha kwanza kama Ibrahim Bacca, Prince Dube na Depu ambao walikosa mechi za mwisho kabla ya mapumziko ya kalenda ya FIFA.

Mtanange huo unatarajiwa kupigwa saa 12:30 jioni ukiwa miongoni mechi tatu za ligi kuu zitakazopigwa leo.

Mashujaa Fc wataumana na Pamba Jiji katika mchezo utakaopigwa saa 10 jioni huku Namungo Fc wakimenyana na JKT Tanzania katika mchezo utakaopigwa saa 3 usiku.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’