Huyu Damaro anawatesa sana

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 Mar 2026
Huyu Damaro anawatesa sana

Inaelezwa Klabu ya Simba SC hivi karibuni ilifungua malalamiko rasmi kupinga uhalali wa uraia wa kiungo wa Yanga, Mohamed Damaro Camara, akidaiwa kusajiliwa kama mchezaji wa ndani bila kufuata taratibu stahiki.

Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa, shauri hilo limefikishwa katika Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kwa ajili ya uchunguzi zaidi, huku Simba wakieleza kuwa mchezaji huyo alihusishwa awali na uraia wa Guinea katika mifumo ya kimataifa ya soka.

Simba wanadai kuwa ili mchezaji atambulike rasmi kubadili uraia wa kisoka, anatakiwa kufuata taratibu za FIFA, ikiwa ni pamoja na kupata kibali maalum cha kubadilisha uwakilishi wa taifa, jambo ambalo wanadai halijathibitishwa kwa Damaro.

Hata hivyo, hoja kubwa iliyoibua mjadala kwa wadau wengi ni muda wa kuibuliwa kwa malalamiko hayo, ikizingatiwa kuwa mchezaji huyo Mamlaka ya uhamiaji nchini ilimtangaza kupata uraia wa Tanzania msimu uliopita wakati akiitumikia Singida Black Stars.

Yanga ilimsajili mwezi Januari kwenye usajili wa dirisha dogo akiwa tayari ni raia wa Tanzania. TFF ikathibitisha uhamisho wake kujiunga na Yanga kama Tanzania.

Klabu ya Yanga imesisitiza kuwa usajili wa mchezaji huyo ulifanyika kwa kuzingatia taratibu za ndani zilizopo. 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’