Mlinzi wa kulia wa Yanga Israel Mwenda ni miongoni mwa mabeki vinara wa 'kutengeneza' mabao katika ligi kuu ya NBC msimu huu.
Mwenda ambaye kwa sasa amejimilikisha nafasi kwenye kikosi cha Wananchi akiwaweka nje Yao Kouassi na Kibwana Shomari, ametoa asisti 3 mpaka sasa. Yuko nyuma ya Ibrahim Imoro wa Singida Black Stars ambaye ametoa asisti nne.
Mkufunzi wa Yanga Pedro Goncalves ameendelea kumuamini Mwenda kwenye kikosi chake licha ya presha anayopata kutoka kwa mashabiki ambao wanatamani kumuona Yao 'Jeshi' akipata nafasi zaidi hasa baada ya kuwa amepona majeraha.
Hata hivyo Mwenda hajamuangusha Goncalves, namba zake kwenye upishi wa mabao zinazungumza.

Yao ameendelea kupata dakika chache kwenye baadhi ya mechi Goncalves akieleza sababu anamtumia kwa tahadhari ili kumuepusha na madhara kwani bado hajaimarika kwa asilimia 100.
Yao alikaa nje ya uwanja kwa takribani miezi 7 baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti mwishoni mwa msimu uliopita