Baada ya jana mlinzi wa pembeni wa Azam FC, Gadiel Michael kufunguka kuwa timu hiyo 'inamkataa', baada ya kubaini amesaini mkataba wa awali kujiunga na Yanga, uongozi wa Yanga umekutana na General Maneja wa Azam FC Abdul Mohammed.
Sasa Azam iko tayari kumalizana na Yanga juu ya Gadiel na huenda usajili wa mchezaji huyo ukakamilishwa rasmi baada ya mazungumzo na kisha taratibu za usajili kukamilika.
Huo ndio uungwana kwenye soka. Vijana hawa kazi yao ni kucheza soka, sasa tukiamua kuwakomoa sababu tu hawataki kucheza timu zetu tutakuwa hatuwatendei haki.
Pia wachezaji wa Kitanazania imefika wakati waanze kuwa na Mawakala au Wanasheria watakaosimamia vyema maswala ya mikataba yao.
Mchezaji hapaswi kulumbana na timu yake kama ana uongozi thabiti unaomsimamia. Nafahamu Gadiel amelazimika kufanya hicho alichofanya kwa kuwa hakuwa na watu wa kumsimamia.

ADVERTISE HERE