Yanga Soccer School kwa kushirikiana na EMWANI CAFE leo wametangaza mashindano maalum ya Vijana wenye vipaji vya soka chini ya miaka 18 yatakayofanyika siku ya Jumamosi tarehe 28 Machi 2026 kwenye kituo cha TFF Kigamboni.
Vijana 10 bora watapewa nafasi ya kujiunga na Yanga Soccer School chini ya EMWANI.
Zawadi kwa washindi:
- Mshindi wa kwanza: Kombe + TSH 3,000,000
- Mshindi wa pili: TSH 1,000,000
- Timu 2 zitakazofika nusu fainali: TSH 500,000 kila moja
Jinsi ya kujisajili:
- Pata fomu Makao Makuu, Jangwani, Dar Es Salaam au tuma maombi kupitia: Info@yangasc.africa
ADVERTISE HERE