Klabu ya Yanga imethibitisha kuwa leo Jumatatu, March 23 2026, Rais wa klabu na Mwenyekiti wa umoja wa vilabu barani Afrika (ACA) Injinia Hersi Said ataongoza kikao maalum cha Kamati ya utendaji.
Kikao hicho ni maalum kwa ajili ya kufanya tathimini ya timu baada ya kukamilika mzunguko wa kwanza Ligi Kuu ya NBC msimu huu.
Kikao hiki kinafanyika Makao Makuu ya Klabu ya Yanga, Jangwani Jijini Dar Es Salaam.
Hatma ya Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves huenda ikafahamika baada ya kikao hicho.
Goncalves , Kocha msaidizi Matthew silva pamoja na kocha wa magolikipa Fernando Pereira wameshiriki katika kikao hicho.

Licha ya kukumbana na changamoto kadhaa kwenye duru ya kwanza, Yanga imepania kutetea ubingwa wa ligi kuu ya NBC kwa msimu wa tano mfululizo.
Wananchi wako kileleni mwa msimamo wa ligi na wamepania kusalia katika nafasi hiyo hadi mwishoni mwa msimu.