Yanga inakimbiza kivuli chake

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Mar 2026
Yanga inakimbiza kivuli chake

Wakati tetesi zikiendelea kushika kasi juu ya hatma ya kocha mkuu wa Yanga Pedro Goncalves, ni wazi wananchi wanahitaji kutumia vyema kipindi hiki cha mapumziko ya FIFA kujiimarisha ili warejee wakiwa imara zaidi.

Licha ya kuendelea kuwa kileleni mwa msimamo wa ligi, mwenendo wa mabingwa hao wa nchi katika mechi za karibuni umewapa mashaka mashabiki ambao wanaamini kama hakutakuwa na mabadiliko huenda msimu huu wakawa na kazi ngumu ya kutetea ubingwa wao.

Ukiacha changamoto ya mejeruhi na ratiba ngumu, malalamiko yalianza mapema tangu wakati kikosi kinashiriki michuano ya ligi ya mabingwa.

Mpaka sasa baada ya kucheza mechi 16 za ligi, Yanga iko nyuma ya kile walichofanya msimu uliopita. Wamekusanya alama 38 alama 4 pungufu ya zile walizokusanya msimu uliopita katika nyakati kama hizi

Msimu uliopita Yanga ilitwaa taji la ligi kuu na pointi 82 baada ya kucheza jumla ya mechi 30, ikishinda 27, sare moja na kupoteza mbili, huku ikifunga mabao 83 yakiwa mengi zaidi kuliko timu nyingine na kuruhusu kumi, ambayo ni machache zaidi.

Hata hivyo mpaka sasa Yanga imedondosha alama 10 katika mechi 16, wakati msimu uliopita walidondosha alama nane tu katika mechi 30.

Yanga imetoka sare tano dhidi ya Mbeya City, Simba, TRA Unted, Azam na Mtibwa Sugar na hivyo kudondosha idadi hiyo ya pointi wakati msimu uliopita timu hiyo ilitoka sare mchezo mmoja pekee dhidi ya JKT Tanzania na ikapoteza michezo miwili dhidi ya Azam na Tabora United (TRA).

Mabosi wa Yanga wanatarajiwa kukutana kujadili mwenendo huo wa timu na haitashangaza yakifanyika mabadiliko kwenye benchi la ufundi.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
3h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
18h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
22h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’