Kikosi cha Yanga kimerejea jijini Dar es salaam wakitokea mkoani Dodoma ambako jana walikamilisha mchezo wa raundi ya 16 ligi kuu ya NBC dhidi ya Mtibwa Sugar.
Mchezo huo uliopigwa uwanja wa Jamhuri, ulimalizika kwa timu hizo kugawana pointi matokeo yakiwa sare ya bao 1-1.
Baada ya kurejea Dar, wachezaji wa Yanga wamepewa mapumziko ya takribani siku tatu kupumzisha miili baada ya ratiba ngumu wakicheza mechi 7 katika kipindi cha siku 21.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema wachezaji walioitwa kwenye majukumu ya timu za Taifa nao wamepewa ruhusa kwenda kujiunga na mataifa yao.
Ligi inatarajiwa kusimama kwa takribani siku 10 kupisha kalenda ya FIFA.
ADVERTISE HERE