Jana Yanga ilikuwa Arusha kuwakabili watoza ushuru wa TRA United katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Mchezo huo ulimalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana, lakini unaweza kusema Wananchi watamshukuru mlinda lango Djigui Diarra ambaye kama sio umahiri wake pengine Yanga ingekosa hata iyo alama moja waliyopata.
Shambulizi la dakika za lala salama lililofanywa na TRA United lingeweza kuwapatia bao kama sio umakini na umahiri wa Diarra.
Ama kwa hakika Diarra ameendelea kuwa mkombozi wa Yanga katika nyakati ngumu.
Msimu huu tayari amekusanya 'cleensheet' 9 akiongoza ordha na pia akiisaidia Yanga kukamilisha mechi 15 za duru ya kwanza bila kupoteza mchezo.
Yanga imeruhusu mabao mawili tu katika mechi hizo 15, hizi ni takwimu bora sana kwake na safu ya ulinzi kwa ujumla.
Chini yake Yanga sasa imecheza mechi 35 mfululizo za ligi bila ya kupoteza. Tabora United (sasa TRA United) ndio timu ya mwisho kuifunga Yanga kwenye ligi Novemba 07 2024.