Muda mchache ujao Yanga itashuka uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha kuikabili TRA United katika mchezo wa ligi kuu ya NBC.
Ukiwa ni mchezo wa kukamilisha duru ya kwanza, Yanga imepania kufunga hesabu zake vyema pasipo kupoteza.
Licha ya kupata muda mdogo wa maandalizi kuelekea mchezo huo, ari na morali ya vijana wa kocha Pedro Goncalves iko juu matumaini yakiwa kuondoka na alama zote tatu.
Habari njema kwa Wananchi ni kuwa kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua sasa yuko fit na huenda akaanza kwenye mchezo huo.
Pacome alirejea kikosini kwenye mchezo uliopita dhidi ya Azam Fc, akitumika kwenye dakika 45 za kipindi cha pili.
Mchezo utapigwa kuanzia saa 10 jioni Tukutane uwanjani....!

ADVERTISE HERE