Kikosi cha Yanga msimu huu 2025/26 kimekuwa bora zaidi baada ya mechi 13 za ligi kuu kulinganisha na misimu 10 iliyopita.
Msimu huu Yanga imekusanya alama nyingi zaidi baada ya mechi 13 huku pia ikifunga mabao mengi.
Aidha, Wananchi pia wameruhusu mabao mawili pekee kwenye michezo yao 13 ya mwanzo wa ligi katika kampeni hii, ni mabao machache zaidi kuliko waliyoruhusu kwenye michezo 13 ya mwanzo wa msimu katika misimu kumi iliyopita.
Wakati msimu uliopita Yanga iliweka rekodi ya kutwaa ubingwa kwa kukusanya alama nyingi zaidi (82), katika michezo 13 ya mwanzo Yanga ilikuwa imekusanya alama 33 wakati msimu huu tayari Wananchi wamekusanya alama 35.
Lakini pia mpaka sasa Yanga haijapoteza mchezo ikitoka sare mechi mbili tu wakati msimu uliopita nyakati kama hizi Yanga ilikuwa imepoteza mechi mbili ikiwa imeruhusu mabao sita.
Yanga imecheza jumla ya mechi 33 za ligi bila kupoteza tangu mara ya mwisho ilipopoteza mchezo wa ligi dhidi ya Tabora United (sasa TRA United), Novemba 07 2024.