Goncalves anazitaka alama tatu Dodoma

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Mar 2026
Goncalves anazitaka alama tatu Dodoma

Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo mgumu wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons ambao utapigwa Alhamisi katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari kuelekea mchezo huo, Goncalves amesema Prisons ni timu ngumu ambayo ina kiu ya matokeo mazuri baada ya kutofanya vyema katik mechi zilizopita.

Kocha huyo raia wa Ureno amesema ana imani kubwa na wachezaji wake kuwa watatekeleza mpango mkakati wa mchezo huo wakihitaji ushindi.

“Leo tutakuwa na mazoezi ya Mwisho kujiandaa dhidi ya Tanzania Prisons, akili zetu zinawaza kufanya vizuri tu, tunajua nini tunataka, Kesho tunacheza na timu ngumu ambayo imetoka kupoteza na Simba kisha wakapata Sare dhidi ya Azam, Tuna uhakika kwamba mchezo utakuwa mgumu lakini tupo hapa kwaajili ya alama tatu na tuna imani tutazipata”

“Licha ya changamoto mbalimbali za Majeruhi, Mfano Job, Mzize na wengine, Timu nzima ina Lengo la kupata matokeo mazuri, hivyo kila mtu anafanya jitihada kubwa kutimiza malengo ya klabu."

"Hata hivyo tunawashukuru sana Wananchi kwa kuwa nasi katika kila hali, Tazama ratiba yetu ilivyokuwa ngumu, kila baada ya siku mbili tuna mechi ya kucheza lakini Wananchi hawajawahi kuwa nyuma, wanakuja kutupa sapoti”

“Tuna wachezaji wengi wenye Uwezo mkubwa sana lakini wanaopaswa kuanza ni 11 pekee, ninachofurahi ni kwamba vijana wote wana uelewa mkubwa kuhusu idea zetu tunazowapa, Naamini kila mmoja yupo tayari kwaajili ya kuisaidia timu, Nina imani kesho itakuwa siku ngumu lakini nzuri kwasababu tumekuja kusaka ushindi,” alisema Goncalves

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’