Yanga iko mkoani Singida ambapo kesho Alhamisi, March 05 watashuka uwanja wa Airtel kuwakabili wenyeji wao Singida Black Stars katika mchezo wa ligi kuu ya NBC.
Wananchi leo watafanya mazoezi yao ya mwisho kwenye dimba la Airtel ambalo Wananchi walishiriki hafla ya uzinduzi wake msimu uliopita.
Singida BS ilitangaza viingilio vya mchezo huo jana ambapo kiingilio cha chini ni Tsh 10,000/- na VIP ni Tsh 30,000/-.

ADVERTISE HERE