Kikosi cha Yanga jana kilirejea Dar wakitokea Ruangwa ambako juzi walipata ushindi muhimu wa bao 1-0 dhidi ya Namungo Fc katika mchezo wa ligi kuu ya NBC.
Kocha Mkuu wa timu hiyo Pedro Goncalves akatoa mapumziko ya siku moja kwa wachezaji ukiwa ni mkakati wa kuwapunguzia uchovu baada ya kucheza mechi mfululizo.
Leo Yanga inarejea mazoezini kukamilisha maandalizi tayari kuwakabili maafande wa JKT Tanzania katika mchezo mwingine mgumu utakaopigwa kesho Jumatano katika uwanja wa KMC Complex.
JKT Tanzania ndio vinara wa ligi kuu ya NBC wakiwa na alama 28 baada ya mechi 16 huku Yanga ikiwa nafasi ya pili ikikusanya alama 25 kutoka mechi 9.
Endapo Yanga itashinda mchezo wa kesho maana yake ni kuwa Wananchi watarejea rasmi kileleni mwa msimamo wa ligi huku wakiwa na mechi 6 za viporo