Nguvu hii sasa ielekezwe kwenye kutetea mataji ya ndani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Feb 2026
Nguvu hii sasa ielekezwe kwenye kutetea mataji ya ndani

JS Kabylie walikuwa na bahati kufungwa mabao matatu tu na Yanga katika mchezo wa kuhitimisha hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL) kundi B.

Yanga iliingia kwenye mchezo huo ikiwa na dhamira ya kuibuka na ushindi mnono, zilikuwa dakika 90 za moto kwelikweli.

Licha ya kuwa malengo ya kufuzu robo fainali hayakufanikiwa baada ya Al Ahly na AS FAR 'kubebana' wakitoka suluhu ya bila kufungana, Wanayanga waliridhishwa na kile walichokishuhudia kutoka kwa timu yao.

Kabla ya mchezo huo Yanga ilifunga mabao mawili tu kutoka mechi tano, lakini jana pakee wakafunga mabao matatu huku wakitengeneza nafasi nyingi pengine kuliko mechi zote walizocheza mwanzo.

Mshambuliaji Laurindo Aurelio 'Depu' alikuwa shujaa wa Yanga akifunga mabao mawili moja likiwa la mkwaju wa penati baada ya Pacome Zouzoua kufanyiwa madhambi na mlinda lango wa JSK.

Depu hakuwa amefunga katika mechi tatu zilizopita za ligi ya mabingwa. Mabao aliyofunga katika mchezo huo sasa yanafanya awe amefunga jumla ya mabao matano na kutoa asisti moja katika mechi sita za mashindano yote.

Wananchi wamekosa nafasi ya kwenda robo fainali lakini hawapaswi kuweka vichwa chini kwani wana timu nzuri inyokwenda kuongeza mataji zaidi msimu huu.

Ari waliyomalizana nayo kwenye mchezo dhidi ya JSK inapaswa kuendelea kwenye ligi na kombe la CRDB malengo yakiwa kutetea mataji hayo.

Bila shaka kocha Pedro Goncalves nae amebaini uimara wa kikosi chake, wakati mwingine hatahofia tena kucheza soka la kushambulia zaidi.

Ziko mechi ambazo wengi wanaamini Yanga ingeweza kufanya vyema zaidi kama isingecheza kwa kujihami muda mwingi.

March 1 dabi ya Kariakoo, mchezo wa kwanza wa ligi dhidi ya Simba utapigwa uwanja wa New Amaan Complex. Safari ya kutetea taji la ligi kuu kwa msimu wa tano mfululizo inapaswa kuanza siku hii...!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
3h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
18h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
21h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’