Najivunia sana timu hii - Goncalves

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Feb 2026
Najivunia sana timu hii - Goncalves

Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves amewapongeza wachezaji wake kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JS Kabylie katika mchezo wa kuhitimisha hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika.

Goncalves amesema licha ya vijana wake kutofuzu hatua ya robo fainali, ameridhishwa na kile walichofanya katika michuano hiyo msimu huu akiamini ni mwanzo wa ujenzi timu imara zaidi ambayo itafanya vyema zaidi huko mbeleni.

"Najivunia timu hii, najivunia wachezaji wangu, benchi la ufundi, viongozi na hata mashabiki ambao wamekuwa nasi bega kwa bega katika kila mechi."

"Tunaangalia kile tulichofanya na nini tunapaswa kufanya ili kuhakikisha tunakuwa bora zaidi. Wakati wa maandalizi kuelekea mchezo huu tuliandaa mpango mkakati, wachezaji wangu wametimiza kile walichopaswa kufanya."

"Lakini mwisho wa siku watu watazungumzia tu kuwa hatujaweza kufuzu lakini katika kundi ambalo lina timu tatu kubwa barani Afrika. Binafsi najivunia sana wachezaji wangu kwa kazi nzuri waiyofanya, najivunia sana timu hii."

"Mashabiki wa Yanga na hata mashabiki wengine wa soka Tanzania wanapaswa kujivunia timu hii. Huu ni mpira wa miguu, wanaofanikiwa ni wale ambao wako tayari kushindana. Sisi tuko hapa kushindana na sio kwenye ligi ya mabingwa pekee, tuna jukumu kubwa la kushinda mataji mengine kama ligi kuu na mashindano mengine," alisema Goncalves.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’