Yanga yawasilisha mapendekezo ya uwanja kwa GSM

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Feb 2026
Yanga yawasilisha mapendekezo ya uwanja kwa GSM

Kamati ya Utendaji Yanga ikiongozwa na Rais Injinia Hersi Said leo ilikutana na kampuni ya GSM chini ya Mwenyekiti wake Ghalib Said Mohamed katika kikao maalum kilichofanyika visiwani Zanzibar.

Akizungumza baada ya kikao hicho, Injinia Hersi alisema kilikuwa maalum kuweka mikakati kuelekea kuanza kwa mradi huo wa ujenzi wa uwanja GSM ikiwa ndio kampuni iliyopewa jukumu baada ya kushinda tenda.

Hersi kupitia kikao hicho, amesema Yanga iliwasilisha mahitaji yake katika kukamilishwa kwa mradi huo ambao utashuhudia Yanga ikitimiza ndoto ya muda mrefu ya kumiliki uwanja ambao utatumika na klabu kwa mashindano ya ndani na Kimataifa.

"Siku kadhaa zilizopita tulitoa taswira ya uelekeo wa ujenzi wa uwanja wetu. Baada ya mchakato, tulimpata mwekezaji ambaye atakwenda kujenga uwanja wetu. Mshindi wa zabuni hiyo ni Kampuni ya GSM chini ya Rais wa Makampuni hayo Ghalib Said Mohamed. Leo tumefanya kikao ambacho tumewasilisha kwao mahitaji yetu"

"Tumewasilisha kwa GSM mahitaji uwanja tunaohitaji. Tunatambua yapo madaraja manne ya viwango vya viwanja vya CAF. Daraja la tatu ni uwanja ambao unaweza kuchezewa mpaka hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika. Daraja la nne linaweza kuandaa mpaka hatua ya fainali. Tunalenga kuwa kati ya daraja la tatu na la nne la ubora wa viwanja. Tunahitaji uwanja bora wa kisasa ambayo utamudu mahitaji yote ya kitaifa na kimataifa"

"Tumeshajadili na kupitisha mchoro ambao tunahitaji kujenga uwanja wetu. Tumeridhia kwa pamoja kuwa mchoro huo umekidhi mahitaji yetu na matakwa ya CAF."

"Baada ya leo tunatarajia kuwa na kikao kingine ambacho kinakwenda kujadili gharama zote. Tukishapata gharama na tukaridhia, hatua ni ya mgawanyo wa majukumu na manufaa ya mradi huu kwa pande zote, kisha tunakwena kusaini mkataba na mbia wetu GSM."

"Hatua ya nne itakuwa utekelezaji wa mradi huu. Tunahitaji wiki moja kukamilisha mahitaji na malengo ambayo tumeafikiana leo. Baada ya kikao cha pili kikao cha tatu tunakwenda kuweka historia. GSM amesema siku anayosaini mkataba atahakikisha kazi inaanza mara moja. GSM yupo tayari na anayo hamu kubwa ya kuanza na kukamilisha historia hii kubwa kwa klabu yetu," alisema Hersi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’