Depu, Dube, Mzize kubeba matumaini ya Yanga Zanzibar

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Feb 2026
Depu, Dube, Mzize kubeba matumaini ya Yanga Zanzibar

Yanga Sc itakuwa na kibarua kizito Jumapili hii, Februari 15, itakapokuwa mwenyeji wa JS Kabylie katika mchezo wa mwisho wa Kundi B wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa visiwani Zanzibar.

Huu ni mchezo wa maamuzi kwa Wananchi wanaohitaji ushindi mnono wa mabao mawili au zaidi ili kufufua matumaini yao ya kufuzu hatua ya robo fainali. Matokeo mengine yoyote yatahitimisha safari yao katika michuano hiyo msimu huu.

Yanga inaingia katika mechi hiyo ikiwa imefunga mabao mawili pekee katika michezo mitano iliyopita ya hatua ya makundi. Bao moja lilifungwa na mshambuliaji Prince Dube huku jingine likiwekwa wavuni na beki Ibrahim Bacca.

Takwimu hizo zinaonyesha wazi ukubwa wa mtihani unaowakabili. Baada ya kufunga mabao mawili katika michezo mitano, sasa Yanga inalazimika kufunga zaidi ya mabao hayo ndani ya dakika 90 dhidi ya JS Kabylie. Si kazi rahisi, lakini hiyo ndiyo njia pekee ya Wananchi kujiweka katika nafasi ya kutinga robo fainali.

Pamoja na changamoto ya mabao, Yanga imeonekana kutengeneza nafasi katika michezo yake iliyopita, lakini tatizo limekuwa kwenye umaliziaji. Katika mchezo dhidi ya AS FAR, Yanga ilipata si chini ya nafasi tatu za wazi ambazo zingeweza kuipa ushindi, lakini zilishindwa kutumika ipasavyo.

Macho sasa yataelekezwa kwa safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Laurindo Aurelio ‘Depu’, Prince Dube na Clement Mzize. Washambuliaji hao wanatarajiwa kubeba matumaini ya mashabiki kwa kuhakikisha wanazitumia vyema nafasi zitakazopatikana.

Depu bado hajaonesha makali yake kwenye michuano ya ligi ya mabingwa, hiyo itakuwa nafasi yake kudhihirisha Yanga haikukosea kumsajili kwenye dirisha dogo.

Dube ameonysha hatari yake kwenye mechi za Kimataifa lakini bado changamoto ya kukosa mabao inaendelea kumuandama. Jumapili anapaswa kuwa na ufanisi wa kiwango cha juu ili kuivusha Yanga katika hatua hiyo.

Mzize ndio kwanza amerejea kutoka kwenye majeruhi ya muda mrefu lakini dakika 10 alizocheza katika mchezo dhidi ya AS FAR zimeonyesha yuko tayari kuipambania Yanga siku ya Jumapili.

Yanga itanufaika na kucheza nyumbani mbele ya mashabiki wake visiwani Zanzibar, lakini presha ya kutafuta ushindi wa mabao mengi itaongeza ushindani katika mchezo huo.

Dakika 90 za Jumapili zitaamua hatma ya Wananchi katika Kundi B, huku matumaini yao pia yakiwa mikononi mwa Al Ahly ambao watahitaji kuifunga AS FAR.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’