Jumapili lazima 'kieleweke' New Amaan Complex

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Feb 2026
Jumapili lazima 'kieleweke' New Amaan Complex

Yanga inatarajiwa kurejea leo kutoka Morocco baada ya mchezo wa raundi ya tano ligi ya mabingwa kundi B wakikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa AS FAR.

Baada ya kikosi kurejea, hakutakuwa na muda wa kupoteza kwani vijana wa kocha Pedro Goncalves wanapaswa kuanza maandalizi ya mchezo wa maamuzi dhidi ya JS Kabylie ambao utapigwa Jumapili, Februari 15.

Kimahesabu Yanga bado ina nafasi ya kufuzu robo fainali, pamoja na kuwa watategemea matokeo ya mchezo kati ya Al Ahly dhidi ya AS FAR.

Ushindi kwa Al Ahly utafungua milango kwa Yanga kufuzu lakini Wananchi watahitaji kushinda kuanzia mabao mawili au zaidi ili kunufainaka.

Kazi kubwa ambayo kocha Goncalves atahitaji kuifanya katika siku chache zilizobaki ni kuimarisha safu yake ya ushambuliaji hasa kwenye matumizi ya nafasi.

Katika mchezo dhidi ya AS FAR, kulikuwa na uwezekano wa Yanga kufunga zaidi ya mabao mawili kama washambuliaji wangetumia nafasi kwa usahihi.

Katika mchezo ujao hakutakuwa na lugha nyingine kama Yanga itakosa ushindi, hata kama AS FAR watapoteza dhidi ya Al Ahly watafuzu.

JS Kabylie hawatakuwa na cha kupoteza katika mchezo huo kwani tayari wamepoteza matumaini ya kusonga mbele hivyo hawatarajiwi kuja na mpango wa 'kupaki basi'.

Unatarajiwa kuwa mchezo wa wazi ambao pengine nafasi nyingi zitatengenezwa kwa kila upande.

Washambuliaji Depu, Dube na hata Clement Mzize watahitaji kufanyia kazi eneo la umaliziaji wa nafasi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
9h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
12h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
17h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
21h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’