Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema baada ya timu hiyo kupoteza mchezo dhidi ya AS FAR, sasa wanaweka nguvu kwenye mchezo wa kuhitimisha hatua ya makundi dhidi ya JS Kabylie ambao utapigwa Ijumaa, Februari 13 uwanja wa New Amaan Complex.
Kamwe amesema Yanga ina nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali hivyo watahakikisha wanashinda mchezo huo.
Akizungumza baada ya kukamilika kwa mchezo dhidi ya AS FAR, Kamwe alisema hawakutimiza malengo yao katika mchezo huo lakini sasa wanakwenda kutimiza malengo katika mchezo wa mwisho nyumbani.
"Tumepoteza mchezo leo (jana) lakini bado tuna nafasi ya kufuzu robo fainali, focus yetu sasa tunaelekeza kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya JS Kabylie pae Guantanamo Bay (New Amaan Complex)."
"Yanga tutafuzu kwa kishindo pale Zanzibar, Tunakwenda kuionyesha Afrika maajabu ya Yanga yanafafanaje anapolitaka jambo lake."
"Kwa sasa wanaopiga mahesabu acha wapige kwani hiyo sio shughuli yetu, sisi tunakwenda kufuzu," alisema Kamwe.
Ushindi wa kuanzia mabao mawili kwa bila unaweza kutosha kuipeleka Yanga robo fainali endapo Al Ahly wataichapa AS FAR kwenye mchezo wa mwisho.
Yanga na Al Ahly zitakuwa nyumbani kwenye mechi za mwisho dhidi ya JS Kabylie na AS FAR