Dube kuendeleza makali dhidi ya AS FAR leo?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Feb 2026
Dube kuendeleza makali dhidi ya AS FAR leo?

AS FAR hawajamsahau mshambuliaji Prince Dube kwani ndiye aliyepeleka kilio kwa maafande hao kutoka Morocco katika mchezo wa kwanza uliozikutanisha Yanga na AS FAR uwanja wa New Amaan Complex Wananchi wakiibuka na ushindi wa bao 1-0.

Saa chache zijazo AS FAR watakuwa wenyeji wa Yanga katika mchezo wa raundi ya tano kundi B dimba la Olympic, Rabat.

Huu ni mchezo ambao pengine Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves atamuhitaji tena Dube kufanya kile alichofanya visiwani Zanzibar.

Yanga itaingia kwenye mchezo huo ikihitaji ushindi ili kusafisha njia kuelekea robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika.

Kuna uwezekano mkubwa Goncalves akaboresha kidogo tu kikosi kile kilichoshinda mechi ya kwanza Zanzibar.

Haitashangaza kama Dube ataanza mbele ya Depu. Mshambuliaji huyo raia wa Zimbabwe tayari amekabiliana na mabeki wa AS FAR hivyo anafahamu madhaifu yao.

Mabadiliko mengine yanaweza kushuhudiwa eneo la kiungo Mohamed Damaro akitarajiwa kuanza sambamba na Duke Abuya na pengine Pacome akianza upande wa winga ya kushoto huku Maxi Nzengeli akitarajiwa upande wa kulia.

Pedro anaweza kumuhitaji Allan Okello eneo la namba 10 ili kuhakikisha ubunifu haukosekani eneo la mwisho.

Ukuta wa Yanga hautarajiwi kuwa na mabadiliko, mabeki watatu Dickson Job, Ibrahim Bacca na Bakari Mwamnyeto watakuwa na jukumu la kulinda lango la Wananchi wakisaidiana na kipa Djigui Diarra ambaye amekuwa mhimili wa Yanga katika michuano hii.

Beki wa kushoto huenda Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' akaanza mbele ya Chadrack Boka ambaye mchezo uliopita dhidi ya Al Ahly alikosolewa kwa vile alivyocheza hasa kwenye kipindi cha pili.

Ni mchezo ambao Yanga haipaswi kupoteza ili kujiwekea mazingira mazuri ya kukata tiketi ya robo fainali.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’