Matchday; AS FAR vs Yanga, CAFCL MD5

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Feb 2026
Matchday; AS FAR vs Yanga, CAFCL MD5

Klabu ya AS FAR ya Morocco leo Jumamosi, Februari 7, itakuwa mwenyeji wa Young Africans (Yanga) ya Tanzania katika mchezo wa hatua ya makundi, Kundi B, wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) utakaopigwa kwenye Uwanja wa Olympic mjini Rabat.

Mchezo huo ni wa raundi ya tano ya makundi na unatarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na umuhimu wake katika mbio za kusaka tiketi ya robo fainali.

Katika msimamo wa Kundi B, ushindani bado uko wazi huku timu zikipigania nafasi mbili za juu zitakazowezesha kufuzu hatua inayofuata. Yanga na AS FAR zinaingia katika mchezo huo zikiwa na pointi zinazozifanya ziwe kwenye presha ya kutafuta ushindi ili kujiweka katika mazingira mazuri kabla ya raundi ya mwisho.

Matokeo ya leo yanaweza kubadili kabisa mwelekeo wa kundi hilo. Ushindi kwa upande wowote utaiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu robo fainali, huku matokeo mengine yakiongeza presha kuelekea mchezo wa mwisho wa makundi.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Tanzania, Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0, matokeo yanayoongeza mvuto wa pambano la leo. AS FAR watakuwa na hamu ya kulipa kisasi nyumbani mbele ya Yanga ambayo ina rekodi nzuri ya kufanya vizuri ugenini.

Ikumbukwe mchezo huo utachezwa bila mashabiki AS FAR wakitumikia adhabu ya CAF kufuatia vurugu za mashabiki wao kwenye mchezo dhidi ya Al Ahly.

Yanga, chini ya kocha Pedro Goncalves, wanaelewa wazi umuhimu wa mechi hiyo. Ushindi ugenini dhidi ya wapinzani wenye uzoefu kama AS FAR utakuwa hatua kubwa kuelekea robo fainali na uthibitisho wa uimara wao katika michuano hiyo.

Kwa upande wa AS FAR, timu hiyo imekuwa na rekodi nzuri wanapocheza nyumbani katika mashindano ya kimataifa, jambo linalofanya mchezo huo kutotabirika kutokana na ubora wa kila timu.

Kwa ujumla, pambano la leo linatajwa kuwa la maamuzi kwa timu zote mbili. Yanga wanahitaji ushindi au angalau sare ili kuendelea kuwa kwenye reli ya kufuzu, wakati AS FAR wakihitaji ushindi ili kujihakikishia nafasi nzuri kabla ya mchezo wa mwisho wa kundi.

Dua za mashabiki wa Yanga na Watanzania kwa ujumla ni kuwaombea wawakilishi hao wa nchi waibuke na ushindi ugenini na kama haitawezekana basi hata sare itafaa.

Ikumbukwe ni Yanga pekee yenye nafasi ya kuendelea kupeperusha bendera ya Tanzania hatua ya robo fainali kama itafanya vyema katika mchezo huo kwani watani zao Simba tayari wamepoteza matumaini ya kufuzu.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
10h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
15h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
19h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
20h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
20h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’