Ni rasmi aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Yanga Ecua Celestin amejiunga na klabu ya JS Kabylie ya Algeria kwa mkopo.
Ecua ataitumikia Kabylie hadi mwishoni mwa msimu huku kukiwa na makubaliano ya kumnunua moja kwa moja kama wataridhishwa na kiwango chake.
Kabylie wamethibitisha usajili wa nyota huyo raia wa Chad akitambulishwa rasmi.
Yanga imelazimika kumtoa Ecua kwa mkopo baada ya kushindwa kufikia matarajio.
Yeye na Mohamed Doumbia wamewapisha nyota wapya waliosajiliwa katika dirisha hili Depu na Allan Okello.
Doumbia amejiunga na Marumo Gallants ya Afrika Kusini.
ADVERTISE HERE