Mzabuni wa ujenzi wa uwanja Yanga kutangazwa Jumamosi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Jan 2026
Mzabuni wa ujenzi wa uwanja Yanga kutangazwa Jumamosi

Klabu ya Young Africans (Yanga SC) inatarajiwa kutangaza rasmi kampuni itakayoshinda zabuni ya ujenzi wa uwanja wake mpya uliopangwa kujengwa eneo la Jangwani, Dar es Salaam, siku ya Jumamosi Januari 31, 2026.

Tangazo hilo linatarajiwa kufanywa mara baada ya mkutano maalum wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo, ambao umeandaliwa mahsusi kujadili ajenda moja tu, ujenzi wa uwanja wa Yanga.

Hayo yameelezwa na Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ali Kamwe, aliyesema kuwa baada ya kikao hicho, jina la mzabuni litatajwa hadharani.

“Mkutano wa Kamati ya Utendaji utajadili kwa kina suala la uwanja wa klabu, na mara baada ya kikao kumalizika, tutawatangazia wanachama na mashabiki kampuni iliyochaguliwa kushirikiana na Yanga katika mradi huu mkubwa,” alisema Kamwe.

Hatua hiyo ni mwendelezo wa mchakato ulioanza wiki chache zilizopita ambapo Yanga ilitangaza rasmi mwito kwa makampuni ya ndani na nje ya nchi kuwasilisha maombi ya zabuni, kwa kuzingatia mpango wa ujenzi wa uwanja uliowekwa wazi na klabu. Makampuni hayo yaliombwa kuonyesha uwezo wa kifedha, uzoefu wa kiufundi na mpango wa utekelezaji wa mradi huo.

Ujenzi wa uwanja wa Yanga Jangwani ni moja ya ndoto kubwa za muda mrefu za wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kongwe nchini. Eneo la Jangwani lina historia ya kipekee kwa Yanga, kwani hapo awali klabu ilikuwa na uwanja wake katika eneo hilo.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
16h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
21h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’