Klabu ya Raja Casablanca ya Morocco inadaiwa kutuma ofa kwa ajili ya kumsajili kiungo wa Yanga Moussa Balla Conte.
Awali Yanga ilikuwa na mpango wa kumtoa Conte kwa mkopo lakini sasa ni kama mpango huo umebadilika baada ya nyota huyo raia wa Guinea kuanza kuonyesha makali yake.
Hata hivyo uongozi wa Yanga sasa utapaswa kuamua hatma yake huku mchezaji mwenyewe akionyesha utayari wa kuelea Raja CA baada ya mwanzo mgumu na Yanga.
Raja CA inanolewa na Fadlu Davids aliyekuwa kocha wa Simba kabla ya kuondoka mwanzoni mwa msimu huu.
Wakati Yanga inamsajili Conte kutoka klabu ya CS Sfaxien ya Tunisia, ilipata upinzali mkali kutoka kwa watani zao Simba, kwani Fadlu alimuhitaji mchezaji huyo katika kikosi chake.
Lakini kwa sasa ni kama Yanga imefunga usajili katika dirisha hili hivyo huenda isiwe rahisi kumruhusu Conte aondoke.