Al Ahly dhidi ya Yanga haijawahi kuwa mechi nyepesi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Jan 2026
Al Ahly dhidi ya Yanga haijawahi kuwa mechi nyepesi

Licha ya rekodi kubwa na ya kutisha ya Al Ahly kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL), klabu ya Young Africans (Yanga) haijawahi kuingia uwanjani ikiwa na hofu kila timu hizi zinapokutana.

Takwimu za mikutano ya nyuma kati ya miamba hiyo miwili zinatoa taswira halisi ya ushindani mkali unaotarajiwa kushuhudiwa leo kwenye uwanja wa Borg El Arab, Alexandria, Misri, katika mchezo wa hatua ya makundi wa CAFCL.

Ukiondoa kipigo cha mabao 3-0 ambacho Yanga ilikipata mwaka 2009, mikutano mingine yote kati ya timu hizo imekuwa ya ushindani mkubwa, ikiisha kwa sare au mshindi kupatikana kwa tofauti ya bao moja pekee.

Mwaka 2023, Yanga na Al Ahly ziliwekwa katika kundi moja (D), hali inayofanana na msimu wa sasa. Katika mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es Salaam, timu hizo ziligawana pointi baada ya kutoka sare ya bao 1-1, kabla ya Al Ahly kushinda kwa bao 1-0 katika mchezo wa marudiano uliopigwa nchini Misri.

Msimu huo wa 2023, Al Ahly na Yanga ndizo timu zilizofanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali, na hadi sasa msimu huu, zinaendelea kupambana kileleni mwa kundi B kuwania tiketi mbili za kufuzu hatua inayofuata.

Historia hii inaongeza mvuto wa pambano la leo, huku Yanga ikisaka kuandika ukurasa mpya wa historia dhidi ya mabingwa wa kihistoria wa Afrika.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’