Alama tatu inawezekana Misri

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Jan 2026
Alama tatu inawezekana Misri

Kikosi cha Al Ahly msimu huu unaweza kusema 'hakitishi' kulinganisha na misimu iliyopita na pengine hii inaweza kuwa nafasi kwa mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga kufanya jambo kubwa huko Misri.

Ni katika mchezo wa raundi ya tatu kundi B ligi ya mabingwa barani Afrika ambapo kesho IJumaa Al Ahly watakuwa wenyeji wa Yanga katika mtanange utakaopigwa saa 1 usiku.

Mabingwa hao wa kihistoria ligi ya mabingwa, wanashika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu ya Misri wakiwa nyuma ya Ceramic na Pyramids.

Katika mechi tano zilizopita kwenye mashindano yote, wameshinda mchezo mmoja tu. Ni sahihi kusema hawako na fomu nzuri.

Upande wa Yanga imetoka kutwaa taji la Mapinduzi na juzi kuilaza Mashujaa Fc mabao 6-0 katika mchezo wa ligi kuu ya NBC. Yanga ilitua Alexandria jana huku kikosi kikiwa na morali kubwa kuelekea mchezo huo.

Hata hivyo hautakuwa mchezo mwepesi kwani Al Ahly wanapocheza kwenye michuano ya ligi ya mabingwa huwa timu tofauti. Ndio maana wametwaa taji hilo mara nyingi zaidi (12) kuliko timu yoyote Afrika.

Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves ameweka wazi malengo ya kikosi chake kuelekea mchezo huo ambapo amesema wanatambua wanakwenda kucheza na timu bora zaidi Afrika hivyo watachukua tahadhari.

Endapo Yanga itashinda au hata kuondoka na alama moja Misri basi itajiweka katika nafasi nzuri kuelekea mchezo wa mrudiano ambao utapigwa wiki ijayo visiwani Zanzibar.

Al Ahly ndio vinara wa kundi B wakiwa na alama nne baada ya mechi mbili sawa na Yanga wao wakifunga mabao mengi zaidi.

Wanakwenda kukutana na Yanga ambayo msimu huu imeweka malengo makubwa ya kufanya vyema katika michuano ya ligi ya mabingwa (CAFCL)

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
13h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’