Huyu Okello ni mali

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Jan 2026
Huyu Okello ni mali

Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves jana kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mashujaa Fc, alimtumia dakika zote 90 kiungo mshambuliaji Allan Okello.

Okello amejiunga na Yanga katika dirisha hili akitokea klabu ya Vipers Fc ya Uganda. Mchezo wake wa kwanza Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 6-0.

Katika mchezo huo, Okello alikuwa mchezaji pekee miongoni mwa waliotua kwenye dirisha dogo ambaye alicheza kwa dakika zote 90.

Hiyo inatosha kuonyesha imani aliyonayo Goncalves kwa kiungo huyo fundi ambaye ujio wake unakwenda kuwarahisishia kazi washambuliaji wa Yanga.

Unaweza kusema sasa Yanga imeziba pengo la Stephane Aziz Ki baada ya kumpata Okello.

Katika mchezo dhidi ya Mashujaa Fc alitengeneza nafasi nne moja ikiwa adimu kwa Duke Abuya huku mpira wake wa faulo dakika za lala salama ukimaliziwa na Depu baada ya mlinda lango Erick Johora kutema.

Okello hajahitaji muda kudhihirisha kipaji chake, bila shaka mengi mazuri yanakuja..!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’