Yanga tayari kuifuata Al Ahly Jumatano

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Jan 2026
Yanga tayari kuifuata Al Ahly Jumatano

Baada ya ushindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya Mashujaa Fc katika mchezo wa ligi kuu jana, kikosi cha Yanga hakina muda wa kupoteza kwani leo wanarejea mazoezini kukamilisha maandalizi kabla ya safari ya Misri.

Alfajiri ya kesho Jumatano Januari 21, Yanga itaondoka nchini kuelekea Misri tayari kwa mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Ahly.

Mechi hiyo ya raundi ya tatu kundi B, itapigwa Ijumaa Januari 23 katika mji wa Alexandria dimba la Borg El Arab. 

Wenyeji Al Ahly wamechagua kupeleka mchezo huo Uwanja wa Borg El Arab uliopo Alexandria ikiwa ni mwendo wa wastani wa saa nne kutoka Cairo kwa usafiri wa treni au basi.

Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves amesema wamejipanga kupata matokeo mazuri dhidi ya Al Ahly licha ya kukiri utakuwa mchezo mgumu.

Al Ahly na Yanga kila moja imekusanya alama nne kundi B baada ya kushinda na kutoka sare mchezo mmoja.

Timu hizo zitachuana katika dakika 90 za kwanza Misri na kurudiana wiki ijayo visiwani Zanzibar.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
19h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’