Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewahakikishia Wananchi kuwa usajili wa mlinda lango Hussein Masalanga ni maalum kuziba nafasi ya Aboubakar Khomein ambaye ni majeruhi.
Kamwe amesema Khomein amepata majeraha ambayo yatamuweka nje kwa miezi mitatu hivyo uamuzi wa kumsajili Masalanga umezingatia ushauri wa benchi la ufundi.
Kamwe amesisitiza Masalanga hajasajiliwa kuchukua nafasi ya Djigui Diarra, kwani Diarra haendi kokote.

"Kwa mujibu wa taarifa ya kitabibu, golikipa wetu Aboubakar khomein amepata majeraha ambayo yatamuweka nje kwa takribani miezi mitatu"
"Hivyo usajili wa Masalanga umefanyika kwa kuzingatia ushauri wa benchi la ufundi na mahitaji ya timu. Khomein ataendelea kusalia Yanga lakini ataondolewa kwenye mfumo nafasi yake itachukuliwa na Masalanga."
"Sasa ifahamike magolikipa wetu watatu ni Djigui Diarra, Aboutwalib Mshery na Hussein Masalanga."
"Diarra bado yupo sana na tayari yuko kambini Avic Town," alisema Kamwe
Katika hatua nyingine, Kamwe amesema bado utambulisho wa mchezaji mmoja...!