Mlinda lango wa Yanga Djiguo Diarra amerejea nchini kuendelea na majukumu yake na mabingwa hao wa soka Tanzania Bara.
Diarra ameacha gumzo Morocco akiingoza Mali kufika robo fainali ya michuano ya Afcon 2025 ambapo waliondolewa na Senegal wakifungwa bao 1-0.
'Mdaka mishale' ataungana na kikosi cha Yanga jijini Dar es salaam kukamilisha maandalizi kabla ya kuelekea Misri kuifuata Al Ahly.
Januari 23 Yanga itakuwa ugenini kumenyana na mabingwa hao wa kihistoria wa ligi ya mabingwa katika mchezo wa raundi ya tatu kundi B.
Timu hizo zitarudiana tena wiki moja baadae visiwani Zanzibar katika mchezo wa raundi ya nne.
Yanga inahitaji kufanya vyema katika mechi zote mbili ili kuweka hai matumaini ya kufuzu hatua ya robo fainali.
ADVERTISE HERE