Kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Uganda Allain Okello anatarajiwa kuwasili nchini siku ya Jumatatu, Januari 12 kuanza majukumu yake na klabu ya Yanga, imefahamika.
Rais wa Yanga Injinia Hersi Said jana alikamilisha usajili wa kiungo huyo fundi baada ya mzungumzo ya kina na Rais wa Vipers Fc, Laurence Mulindwa.
Mazungumzo hayo pia yalifungua ushirikiano mpya kati ya Yanga na Vipers Fc katika masuala yanayohusiana na mpira wa miguu.
Okello anatajwa kusaini mkataba wa miaka miwili na nusu kuitumikia Yanga. Amekamilisha idadi ya nyota watano waliosajiliwa na Yanga katika dirisha hili.
Wengine ni Emmanuel Mwanengo, Mohamed Damaro, Mauruf Tchakei na Laurindo Aurelio 'Depú'
ADVERTISE HERE