Yanga leo inahitimisha hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Mapinduzi kwa mchezo dhidi ya TRA United utakaopigwa saa 2:15 usiku katika uwanja wa New Amaan Complex.
Baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya KVZ katika mchezo uliopita, leo Yanga inahitaji matokeo angalau alama moja tu ili kutinga nusu fainali.
Tangu mechi ya kwanza, mkufunzi wa Yanga Pedro Goncalves alionyesha wazi analitaka kombe akitumia kikosi chake kamili, bila shaka leo Wananchi wanatarajia mwendelezo huo mbele ya TRA United.
Kama Yanga itatinga nusu fainali, katika hatua hiyo itamenyana na Singida Black Stars huku watani zao Simba wakitarajiwa kuchuana na Azam Fc katika mchezo wa nusu fainali.
Fainali za michuano hiyo mwaka huu zitahusisha timu zote kutoka Tanzania Bara
ADVERTISE HERE