Kikosi cha Yanga leo kitashuka dimba la New Amaan Complex kuikabili KVZ katika mchezo wake wa kwanza hatua ya makundi kombe la Mapinduzi.
Yanga ilitua Zanzibar mapema jana na jioni kikosi kikapata nafasi ya kukamilisha maandalizi yake visiwani humo.
Mkufunzi wa Yanga Pedro Goncalves amesema atautumia mchezo huo kuwapa nafasi nyota wapya waliosajiliwa katika dirisha hili.
KVZ tayari wamecheza mechi moja dhidi ya TRA United ambayo ilimalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana.
Kama Yanga inashinda mchezo wa leo basi itahitaji hata sare tu kwenye mchezo wa pili dhidi ya TRA United ili kutinga nusu fainali.
ADVERTISE HERE