Mlinda lango wa Yanga Djigui Diarra jana akiwa katika majukumu ya timu yake ya Taifa Mali, alidhihirisha pengine ndio golikipa namba moja barani Afrika kwa sasa baada ya kuibeba Mali kuipeleka robo fainali ya michuano ya Afcon 2025 mbele ya Tunisia.
Mchezo huo ambao uliamuliwa kwa changamoto ya mikwaju ya penati baada ya sare ya bao 1-1, Mali waliibuka na ushindi wa penati 3-2 huku Diarra akiokoa mikwaju miwili.
Diarra ameendelea kudhihirisha ubora wake akiondoka na tuzo ya nyota wa mchezo huo.

Leo nyota wengine wa Yanga Ibrahim Bacca, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto na Mohamed Hussein watakuwa uwanjani pale Tanzania itakapomenyana na Morocco
ADVERTISE HERE