Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limeiadhibu klabu ya AS FAR kucheza mechi mbili bila ya mashabiki kufuatia matukio ya vurugu za mashabiki yaliyojitokeza wakati wa mchezo wao wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Ahly.
Timu hiyo kutoka Morocco pia imepigwa faidi ya dola 100,000 ambayo wanapaswa kulipwa ndani ya kipindi cha siku 60.
Mechi mbili ambazo AS FAR watacheza nyumbani bila ya mashabiki ni dhidi ya JS Kabylie na Yanga.
Hii inaweza kuwa habari njema kwa Wananchi ambao watakwenda Morocco baada ya mechi mbili dhidi ya Al Ahly zitakazopigwa mwishoni mwa Januari 2026 na mwanzoni mwa Februari.
CAF pia wameiadhibu JS Kabylie kwa kuipiga faini ya dola 35,000 kufuatia matukio ya vurugu kwenye mchezo dhidi ya Yanga.
ADVERTISE HERE