Mikiki mikiki ya ligi kuu ya Wanawake inaendelea leo ambapo kinadada wa Yanga Princess watakuwa dimba la Azam Complex kuikabili Gaita Queens.
Ni mchezo wa mzunguuko wa nne, kinadada Wananchi wakipania kuendeleza rekodi ya ushindi wa asilimia 100 ili kuendelea kusalia katika nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi.
Yanga Princess imeshinda mechi zote tatu zilizopita kama ilivyokuwa kwa wapinzani wake kwenye mbio za ubingwa JKT Queens na Simba Queens.
Hii hapa ratiba ya mechi za mzunguuko wa nne;

ADVERTISE HERE