Yanga kuhitimisha mazoezi leo, kwenda mapumziko ya Christmas

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Dec 2025
Yanga kuhitimisha mazoezi leo, kwenda mapumziko ya Christmas

Kikosi cha Yanga leo kitahitimisha mazoezi na wachezaji kurejea makwao kuungana na familia zao kwa ajili ya sikukuu ya Christmas.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema wachezaji watakuwa na mapumziko ya wiki moja ambapo watarejea tena mazoezini Disemba 28 kuendelea na maandalizi ya ratiba ya mechi zitakazofuata.

"Tumekuwa na wiki nzima ya mazoezi wachezaji wanakwenda kwenye 'break' nyingine ili kutoa nafasi kwa wachezaji kwenda kusherehekea sikukuu ya Christmas karibu na familia zao".

"Tarehe 28 wachezaji wataripoti tena kambini ambapo wakirudi tunaanza maandalizi na mchakamchaka kwa ajili ya mechi za ligi kuu ya mashindano mengine," alisema Kamwe.

Yanga ni miongoni mwa timu nane ambazo zimethibitisha kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi inayotarajiwa kuanza Disemba 29.

Hata hivyo huenda kocha mkuu wa Yanga Pedro Goncalves akatumia wachezaji wachache kutoka kikosi cha kwanza akiwaongezea wengine kutoka timu ya vijana.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’