Singida BS wamtaka Assink baada ya kung'ara Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Dec 2025
Singida BS wamtaka Assink baada ya kung'ara Yanga

Baada ya kung'ara katika mechi mbili za ligi kuu dhidi ya Fountain Gate na Coastal Union, klabu ya Singida Black Stars imeanza mchakato wa kumrejesha beki wa kati Frank Assink ambaye anaitumikia Yanga kwa mkopo, imefahamika.

Assink alitua Yanga kwa mkopo katika dirisha lililopita siku chache kabla ya dirisha hilo kufungwa akichukua nafasi ya Yao Kouassi ambaye hakuwa tayari kurejea uwanjani baada ya kufanyiwa upasuaji.

Inaelezwa mkufunzi wa Singida BS Miguel Gamondi amewaagiza mabosi wa timu hiyo kumrejesha kikosini ili kuimarisha safu yake ya ulinzi ambayo kwa mechi za karibuni imeonekana kusuasua.

Hata hivyo ni wazi Yanga itapambana kumbakisha Assink ambaye alinza msimu taratibu lakini kwa sasa ameonekana kumshawishi kocha Pedro Goncalves ambaye alimtumia kwa dakika zote 180 kwenye mechi mbili zilizopita.

Baada ya michuano ya Afcon 2025 kuhitimishwa huko Morocco mwishoni mwa mwezi ujao, kutakuwa na mfululizo wa mechi katika mashindano yote kwani msimu utapaswa kumalizika katika kipindi cha miezi minne ili kuepusha muingiliano na michuano ya kombe la Dunia itakayoanza Juni 2026

Upana wa kikosi ndio utakaoamua hatma ya kufanya vyema katika mashindano yote

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’