Wakati Yanga ikishuka uwanja wa KMC Complex jioni ya leo kuikabili Fountain Gate katika mwendelezo wa ligi kuu ya NBC, Wananchi watafanya tukio la aina yake kwa ajili ya kumpongeza mlinda lango wao namba moja Djigui Diarra.
Tangu ajiunge na Yanga misimu minne iliyopita akitokea Stade Malien, Diarra ameendelea kuzipata tabasamu nyuso za mashabiki wa Yanga kwa kazi yake nzuri mbele ya milingoti ya goli.
Takwimu zinaonyesha baada ya mchezo dhidi ya JS Kabylie ulioisha kwa suluhu ya bila kufungana, Diarra amefikisha cleansheets tano katika michezo sita aliyocheza msimu huu kwenye ligi ya mabingwa Barani Afrika.
Mchezo pekee ambao Diarra aliruhusu bao, ulikuwa mkondo wa pili dhidi ya Silver Strikers ya Malawi, ambapo mchezo huo Yanga ilipoteza kwa 1-0.
Aidha katika mechi nne za ligi kuu alizokaa langoni Diarra pia ameruhusu bao moja tu akiondoka na cleensheet tatu. Hivyo msimu huu katika mashindano yote, Diarra ameruhusu mabao mawili tu katika mechi 11 akikusanya cleensheet 9.