Tunaheshimu kila mpinzani - Goncalves

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Dec 2025
Tunaheshimu kila mpinzani - Goncalves

Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Fountain Gate ambao utapigwa kesho Alhamisi katika uwanja wa KMC Complex.

Goncalves amesema hakuna mechi nyepesi kwenye ligi hivyo wataingia katika mchezo huo kwa kuwaheshimu wapinzani wao huku akiweka wazi ugumu wa mchezo huo hasa ikizingatiwa Yanga imetoka safari ndefu Algeria walikocheza mechi ya ligi ya mabingwa dhidi ya JS Kabylie na kupata alama moja muhimu.

Hata hivyo amesisitiza Yanga ni timu inayohitaji alama tatu kutoka kila mchezo hivyo wanakwenda kupambana wakiwa na lengo la kushinda mchezo huo.

“Baaada ya kurejea Algeria hatujapata muda mrefu sana wa kujiandaa. Safari ilikuwa ndefu sana. Tunayo changamoto ya kuhakikisha hatutoki nje ya mstari na malengo yetu. Sifa kubwa ya Yanga ni kushinda kila mechi. Haijalishi ni mashindano gani ila kipaumbele chetu ni kushinda tu”

“Tunafanya kazi kwa bidii kubwa mno kuhakikisha tunafanya vizuri na kusahihisha dosari ambazo zimejitokeza. Tunafahamu kuwa wapinzani wetu wamejiandaa vizuri pia. Tunahehsimu kila mpinzani anayekuja mbele yetu. Tutacheza kama vile tunacheza mchezo wa ligi ya Mabingwa. Falsafa yetu haitabadilka. Dhamira yetu ni ushindi tu”

“Tuna baadhi ya wachezaji ambao wanasumbuliwa na maumivu lakini na kuanzia leo nina matumaini. Naweza kusema nina asilimia kubwa ya kikosi ambacho nina kihitaji. Tunaendelea kufanyia kazi changamoto ndogo ndogo za majeraha kwa baadhi ya wachezaji ambazo zinawasumbua ili kuona utayari wao kimwili,” alisema Goncalves

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, mlinda lango Aboubakar Khomain amesema wako tayari na kila mchezaji anafahamu umuhimu wa mchezo huo.

Khomein amewahakikishia mashabiki wa Yanga kuwa watarajie burudani itakayoambatana na ushindi katika mchezo huo.

“Tumemalizana na mechi za ligi ya mabingwa kwa sasa, akili yetu na malengo yetu sasa ni nyumbani hapa. Kila mchezaji anajua nini cha kufanya. Tuliwekeza nguvu kubwa sana kwenye ligi ya mabingwa lakini bado Tupo imara kimwili na kiakili na tupo tayari kupigania alama tatu muhimu kwa mchezo wa kesho.”

“Nichukue nafasi hii kuwaalika Wananchi wote hapo kesho katika uwanja wa KMC, sisi tupo tayari kuwapa burudani ambayo mmeuzoea, mje kwa wingi kutupa sapoti vijana wenu,” alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’