Yanga imeondoka na alama moja muhimu Algeria baada ya matokeo ya suluhu ya bila kufungana dhidi ya JS Kbylie katika mchezo wa pili kundi B.
Katika siku ambayo utawapongeza wachezaji wote kwa nidhamu nzuri katika ulinzi, kocha Pedro Goncalves na benchi lake la ufundi wanastahili kongole kwa kazi kubwa waliyofanya kuiboresha Yanga katika kipindi cha muda mfupi.
Leo nyota wa Yanga walikimbia kwa muda wote wa mchezo huku wakionesha ushirikiano mkubwa kuwadhibiti wapinzani wao.
Ni alama moja muhimu kwa Yanga ugenini ambayo inaipeleka Yanga kileleni mwa kundi B baada ya kufikisha alama 4.
Mashabiki wa JS Kabylie hawakuamini kile walichokishuhudia ndani ya dakika 90, haishangazi kuona wakifanya kwa kumtupia makopo mlinda lango Djigui Diarra wakati mchezo ukiendelea.





Hii ndio Yanga tunayoijua...!