Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya JS Kabylie utakaopigwa kesho Ijumaa huko Algeria.
Akizungumza katika mkutano na wanahabari mapema leo kuelekea mchezo huo, Goncalves alisema wako Algeria kuwania alama tatu.
Licha ya kutambua ugumu wa mchezo huo, Gancalves alisema jambo la uhakika kutoka kwa timu yake ni kuwa wanakwenda kupambana kuzisaka alama tatu.
"Ni mchezo wa pili katika hili kundi gumu zaidi, tumefanikiwa kupata pointi 3 za kwanza nyumbani na kesho tuna mechi nyingine ngumu hapa dhidi ya JS Kabylie."
“Ni mpinzani mgumu sana na ana nguvu kubwa ya mashabiki. Hii ni mara yangu ya nne nakuja hapa Algeria kuwaona JS Kabilie. Ni Klabu yenye hamasa na mashabiki wengi sana”
“Kwetu Yanga ni mazingira mazuri kuwepo hapa, kucheza dhidi ya klabu mbele mbele ya mashabiki wengi pia uwanjani, tumekuja kupambana kupata pointi 3 hapa na sio kitu kingine."
"Kesho ni mechi mpya, mechi tofauti kabisa. Kilichotokea kwenye mechi ya kwanza kimeshapita, akili yetu iko kwenye mchezo wa kesho. Tunajua mazingira yatakavyokua na tuko tayari. Kelele na hamasa za mashabiki wao zinaweza kuwa nguvu kwao na kwetu pia kwa wachezaji wetu kujituma zaidi uwanjani.Tuna mpango wetu na ni muhimu kuusimamia kwa dakika zote uwanjani."
"Nafahamu mashabiki wa JS Kabylie watakuja kwa wingi uwanjani kutazama mchezo huu, niwahakikishie hata sisi tuko hapa kucheza mpira," alisema Goncalves
Yanga inatarajiwa kukamilisha maandalizi yake leo saa 1 usiku katika muda ambao mchezo huo utapigwa hapo kesho