Yanga ilivyocheleweshwa uwanja wa ndege Algeria

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Nov 2025
Yanga ilivyocheleweshwa uwanja wa ndege Algeria

Kikosi cha Yanga kilitua Algeria jana na leo watandelea na mazoezi nchini humo kuelekea mchezo wa pili wa hatua ya makundi CAFCL dhidi ya JS Kabylie ambao utapigwa keshokutwa Ijumaa, Novemba 28.

Hata hivyo baada ya kutua uwanja wa ndege jana, Wananchi walikutana na tukio la aina yake ambapo walilazimika kusubiri kwa takribani masaa matatu baada ya mizigo yao kuzuiwa na mamlaka.

Yanga ambayo ilitua muda mmoja na klabu ya Mamelodi Sundowns iliyo nchini humo kumenyana na MC Alger katika mchezo mwingine wa ligi ya mabingwa, walisubiri mizigo yao hadi pale ilipoachiwa.

Hii ni mbinu inayotumiwa sana miongoni mwa timu kutoka Afrika ya Kaskazini kuwachosha wachezaji kwa kuwaweka uwanja wa ndege muda mrefu.

Baada ya kupata mizigo yao, Yanga ilielekea hotelini na vijana wa kocha Pedro Goncalves hawakuwa na muda wa kupoteza kwani walianza program ya mazoezi ya 'recovery' na leo itakuwa siku ya kwanza ya mazoezi kamili.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’