Alama tatu muhimu nyumbani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Nov 2025
Alama tatu muhimu nyumbani

Kocha Pedro Goncalves leo amemaliza unyonge wa Yanga kwenye mechi za ufunguzi hatua ya makundi michuano ya CAF baada ya kuwaongoza Wananchi kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AS FAR katika mchezo wa CAFCL kundi B.

Ni Mwana Mfalme Prince Dube aliyewapa Yanga alama tatu muhimu nyumbani na kuanza vyema kampeni ya kuisaka robo fainali.

Vijana wa Goncalves leo walionekana kuwa bora zaidi na pengine wangeweza kufunga mabao zaidi kama sio uimara wa mlinda lango wa AS FAR.

Kazi nzuri eneo la katikati ya uwanja Duke Abuya akiendelea kuitendea haki nafasi yake mpya ya kiungo mkabaji huku Pacome Zouzoua akiwa mwiba mkali kwa walinzi wa AS FAR.

Ukuta wa Yanga ulikuwa salama mbele ya Dickson Job na Ibrahim Bacca huku Mohamed Hussein na Israh Mwenda wakifanya kazi nzuri pembezoni mwa uwanja, Dgijui Diarra nae akiiweka Yanga salama kwa kuokoa nafasi kadhaa za hatari.

Kikosi cha Yanga leo kimeonyesha mabadiliko makubwa ya kiuchezaji, ari na morali ya timu kwa ujumla ilikuwa juu wachezaji wakivuja jasho jingi kuhakikisha alama tatu zinabaki nyumbani.

Goncalves anarudi tena uwanja wa mazoezi kukiandaa kikosi chake kwa mchezo unaofuata dhidi ya JS Kabylie utakaopigwa wiki ijayo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’