Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga wameanza kampeni yao katika hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa (CAFCL) wakiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AS FR katika mchezo uliopigwa uwanja wa New Amaan Complex.
Bao la dakika ya 59 lililofungwa na Prince Dube limeihakikishia Yanga alama tatu muhimu ambazo zinawaweka kileleni mwa kundi B
Ilikuwa pasi ndefu iliyopigwa na Mudathir Yahya nyuma ya migongo ya mabeki wa AS FAR ilitendewa haki na Dube ambaye aliwazidi mbio mabeki hao kabla ya kutumbukiza mpira kimiani.
Yanga ilianza mchezo huo kwa kasi na pengine ingeweza kufunga mapema kama sio uimara wa mlinda lango wa AS FAR aliyeokoa takribani michomo mitatu ya hatari.
Ni alama tatu muhimu nyumbani, Yanga ikianza vyema kampeni ya kuisaka tiketi ya robo fainali.
Yalisemwa mengi kabla ya mchezo huo lakini kwa mara nyingine Yanga imedhihirisha iko tayari kucheza na yeyote.
Bravooooooo Wananchiiii....!