Goncalves ana mtihani huu makundi CAFCL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Nov 2025
Goncalves ana mtihani huu makundi CAFCL

Jumapili Novemba 22 katika uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar, Yanga itasukuma kete yake ya kwanza katika hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL) pale watakapoikabili AS FAR, ikiwa ni mechi ya kwanza kundi B.

Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves utakuwa mtihani wake wa kwanza kwenye mechi za Kimataifa baada ya kupokea kijiti kutoka kwa Romain Folz aliyeiongoza Yanga kwenye mechi tatu za awali kabla ya Patrick Mabedi kukabidhiwa jukumu kwa muda kwenye mchezo wa kutinga makundi dhidi ya Silver Strikers.

Katika misimu mitatu iliyopita ambayo Yanga imeshirikia ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho la CAF, haijawa na rekodi nzuri kwenye mechi za ufunguzi.

Msimu wa 2022/23 kwenye michuano ya kombe la Shirikisho (CAFCC) Yanga ilianza kwa kupoteza mchezo wa kwanza ugenini dhidi ya US Monastir ikikubali kipigo cha mabao 2-0 lakini ikashinda mabao 3-1 dhidi ya TP Mazembe katika mchezo uliofuata.

Msimu wa 2023/24 Yanga ikarejea hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa baada ya kusubiri kwa miaka 25, mwanzo haukuwa mzuri.

Katika msimu ambao Yanga ilipangwa kundi D na Al Ahly waliyopangwa nayo kundi B msimu huu, mechi ya kwanza ilizikutanisha timu hizo uwanja wa Benjamin Mkapa na mchezo ukamalizika kwa sare ya bao 1-1 Pacome Zouzoua akiisawazishia Yanga dakika za jioni.

Baada ya mchezo huo Yanga ikaelekea Ghana kuikabili Medeama nako ikalazimishwa sare ya bao 1-1 kisha kupata ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wa marudiano dhidi ya Medeama uwanja wa Benjamin Mkapa.

Ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya CR Belouizdad ndio uliowahakikishia Wananchi kutinga robo fainali iliyoacha kumbukumbu ya aina yake baada ya kuondoshwa kwa utata na Mamelodi Sundowns.

Msimu uliopita 2024/25 jinamizi la kuanza vibaya mechi za hatua ya makundi likaendelea tena pale Yanga ilipokubali kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Al Hilal katika mchezo uliopigwa dimba la Mkapa.

Wananchi wakasafiri Algeria walikokutana na kipigo kingine cha mabao 2-0 dhidi ya MC Alger, unaweza kusema vipigo hivi vilichangia Yanga kukosa nafasi ya kutinga robo fainali pale walipokosa ushindi kwenye mchezo wa maamuzi dhidi ya MC Alger uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kutokana na rekodi ya kutofanya vyema kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, msimu huu Yanga imeamua kucheza mechi zake za nyumbani katika uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar.

Mechi za nyumbani zina umuhimu wa kipekee katika kusaka tiketi ya kufuzu robo fainali. Jukumu la Goncalves ni kuhakikisha Yanga haipotezi alama yoyote nyumbani na kufuta wastani wa rekodi ya metokeo mabaya katika mechi zilizopita

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’