Kuna habari njema kwa mashabiki wa Yanga juu ya mshambuliaji wao Clement Mzize aliyefanyiwa upasuaji wa goti hivi karibuni.
Kuna dalili njema kuwa Mzize huenda akarejea uwanjani mapema kuliko ilivyotarajiwa baada ya kuanza mazoezi mepesi zikiwa ni wiki mbili tangu afanyiwe upasuaji wa goti.
Nyota huyo alitarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa wiki 8 hadi 10 pengine sasa anaweza kurejea mapema zaidi. Juzi alianza program maalum ya mazoezi ikiwa sehemu ya 'recovery'.
Mzize ameandamwa na majeraha tangu kuanza kwa msimu huu, akiumia kwa mara ya kwanza wakati anaitumikia timu ya Taifa kwenye michuano ya CHAN 2024 iliyofanyika mwezi August mwaka huu.
Kwa sasa Yanga inaendelea kuwategemea washambuliaji Prince Dube na Andy Boyeli huku kukiwa na tetesi huenda ikarudi sokoni kwenye dirisha dogo kuongeza mshambuliaji mwingine.