Yanga ni mwendo wa rekodi za kibabe Ligi Kuu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Nov 2025
Yanga ni mwendo wa rekodi za kibabe Ligi Kuu

Ushindi wa mabao 4-1 ambao waliupata Yanga juzi dhidi ya KMC umewapeleka kileleni mwa msimamo wa ligi kwa mara ya kwanza msimu huu baada ya kufikisha alama 10 katika mechi nne walizocheza. Hata hivyo ushindi huo pia umekuja na rekodi za aina yake. 

Katika msimu ambao mijadala mingi inaikosoa Yanga kuwa haichezi vyema, bado ndio timu iliyoanza vyema zaidi msimu ikiwa imefunga mabao tisa na kuruhusu bao moja tu.

Yaani Yanga ndio timu iliyofunga mabao mengi kuliko nyingine ambazo wachambuzi wanazisifia kuwa bora zaidi.

Lakini pia Yanga sasa imecheza zaidi ya siku 368 bila ya kupoteza mchezo wa ligi kuu.

Ndio! Wananchi hawajapoteza mchezo wa ligi kuu ya NBC tangu walipofungwa kwa mara ya mwisho na Tabora United mabao 3-1 pale uwanja wa Azam Complex.

Wakati huu ambao mashambulizi yamekuwa mengi kwa Wananchi, ni wakati pia kwa Yanga kujipanga zaidi ili kuendeleza ubabe.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’